Nunua na kuuza hisa
ukiwa na tozo ya asilimia 0%
Shiriki katika biashara ya kimataifa ya hisa za makampuni maarufu duniani na upate gawio bila tozo zozote.
Kwa nini biashara ya hisa na JustMarkets?
Kuanzia kampuni kubwa za ubunifu wa kiteknolojia hadi kampuni za madawa zinazoongoza, fanya biashara na JustMarkets na uvinjari masoko bora ya hisa ulimwenguni, yaliyolengwa ili kuboresha njia yako ya kufanya biashara.
Aina tofauti tofauti za hisa
Jitumbukize katika soko la hisa ukiwa na aina mbalimbali za nyenzo za kupima mabadiliko ya bei za hisa. Shiriki katika masoko kama fahali au dubu kwa usawa, ukitumia machaguo ya uwezo wa kujiinua ambayo yanaweza kuongezeka hadi 1:20.
Utekelezaji wa oda haraka
Katika JustMarkets, dili zako zinafanywa papo hapo. Ndani ya sekunde tu, tunahakikisha kuwa biashara zako zinatekelezwa, na kukupa kasi unayohitaji ili kufanya biashara kwa ufanisi.
Tofauti Ndogo & Isiyobadilika Badilika kati ya bei ya kununua na kuuza
Nunua na kuuza hisa za Apple(AAPL), Tesla(TSLA), au Spotify(SPOT) kukiwa na tofauti ndogo mno kati ya bei ya kununua na kuuza ikianzia pips 0.1, kuhakikisha utulivu hata wakati ambapo soko linabadilikabadilika mno.
Kutoa fedha papo hapo
Pata pesa zako haraka unapotaka kuzitoa. Chagua kutoka kwenye njia mbalimbali za malipo na upate idhini ya haraka kwa maombi yako.
Ulinzi dhidi ya mabadiliko ya bei yenye athari hasi
Fanya biashara bila wasiwasi ukiwa na ulinzi wetu dhidi ya mabadiliko ya bei yenye athari hasi. Inazuia mabadiliko ya bei yenye athari hasi, kwa hivyo biashara zako huanzia na kuishia pale unapotarajia, bila kukosa mabadiliko yoyote madogo ya bei.
Usalama wa uwekezaji
Wekeza katika hisa zenye ulinzi wa Salio Chini ya Sifuri. Wakati salio linapofika chini ya sifuri kwa sababu ya mabadiliko makubwa ya ghafla kwenye soko, salio litawekwa sifuri ili kuwalinda wateja dhidi ya hasara zisizotarajiwa.
Zana za soko la hisa
Tofauti ya bei wastani
pips
Kamisheni
kwa kila loti/ndani
Dhamana
1:20
Malipo ya usiku mrefu
Pointi
Malipo ya usiku mfupi
Pointi
Kiwango cha kuzuia*
pips
Hali ya soko la hisa
Soko la hisa linatoa jukwaa kubwa la biashara ya kimataifa katika hisa za makampuni. Kwa kufanya biashara ya hisa, unaweza kufaidika na kutokana na kupanda na kushuka kwa bei za hisa, iwe zinaelekea juu au chini.
Saa za kufanya biashara
Hisa za Ulaya zinaweza kununuliwa na kuuzwa kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa kati ya saa 4:05 asubuhi na saa 12:29 jioni. Hisa za Marekani zinaweza kununuliwa na kuuzwa kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa kati ya 10:35 jioni na saa 4:59 usiku.
| Zana | Kufungua | Kufunga |
| Hisa za Umoja wa Ulaya | Jumatatu 10:05 Mapumziko ya kila siku 18:59 – 10:05 |
Ijumaa 18:59 |
| Hisa za Marekani | Jumatatu 16:35 Mapumziko ya kila siku 22:59 – 16:35 |
Ijumaa 22:59 |
Tafadhali kumbuka, unaweza tu kufunga oda zilizo wazi wakati wa saa hizi za kufanya biashara kabla ya soko. Haiwezekani kufungua oda mpya wakati wa kufanya biashara kabla ya soko.
Muda wote uko katika wakati wa seva (GMT+2).
Tofauti kati ya bei za kununua na kuuza
Tofauti kati ya bei ya kununua na kuuza katika soko la hisa mara nyingi hubadilikabadilika. Tofauti kati ya bei za kununua na kuuza zilizotajwa hapo juu ni wastani uliopatikana kutoka katika biashara za siku za awali. Angalia tovuti yetu ili kuona tofauti kati ya bei ya kununua na kuuza kwa sasa.
Tofauti kati ya bei za kununua na kuuza zinaweza kuongezeka wakati wa ukwasi mdogo au mabadiliko makubwa katika soko. Hii inajumuisha nyakati kama vile wakati wa mgeuko wa soko, habari mpya kuhusu soko, na matoleo mapya na inaweza kuendelea hadi hali ya kawaida katika soko itakapoanza tena.
Tofauti zetu bora kati ya bei ya kununua na kuuza ni hakika kwenye akaunti yetu ya Raw Spread, ambapo tofauti kati ya bei ya kununua na kuuza huanzia pips 0.1.
Biashara ya kubadilisha bila riba
Riba ya ubadilishaji ni ada inayotozwa kwenye nafasi za biashara za fedha za kigeni ambazo zinabaki wazi usiku kucha. Riba ya ubadilishaji hutofautiana katika jozi tofauti za sarafu. Riba za ubadilishaji hutozwa saa 4:00 usiku GMT+2 kila siku, bila kujumuisha wikendi, hadi nafasi itakapokuwa imefungwa. Ni muhimu kutambua kwamba kwa biashara yenye jozi za fedha za kigeni, riba za ubadilishaji kwa siku ya Jumatano huongezeka mara tatu ili kugharimia gharama za riba za wikendi.
Hutatozwa kwa hisa zilizowekewa alama ya “Waliokubaliwa Ubadilishaji bila riba wanaruhusiwa” katika jedwali hapo juu ikiwa una hali ya ubadilishaji bila riba.
Akaunti zote za wateja kutoka nchi yoyote hupewa moja kwa moja hali ya ubadilishaji bila riba.
Kiwango cha kusitisha
Kiwango cha amri ya kusimamisha biashara ndio umbali wa chini zaidi unaokubalika kati ya bei unayotaka kufungua nafasi nayo na bei ya sasa ya soko wakati unapoweka oda inayosubiri (kama vile Zuia Hasara, Chukua Faida, Kuuza kwa amri ya kusubiri bei ipande/ Kuuza kwa amri ya kusubiri bei ishuke, au Kipimo cha kunua kwa bei ya chini/ Kipimo cha kuuza kwa bei ya juu). Kiwango hiki husaidia kupunguza hatari ya mabadiliko ya ghafla ya bei (mtelezo wa bei) wakati wa kipindi cha mabadiliko makubwa ya soko, na huhakikisha utekelezaji wa uhakika zaidi wa oda zinazosubiri.
Zingatia kwamba kiasi katika kiwango cha kusitisha kilichoonyeshwa kwenye jedwali hapo juu kinaweza kubadilika na huenda kisiweze kutumiwa na wafanyabiashara wanaotumia mikakati mahususi ya kuchakata oda nyingi haraka au kutumia Washauri Wataalamu.
Matangazo ya kifedha
Kampuni zinapotoa ripoti zao za kifedha, kunaweza kuwa na mtikisiko mkubwa wa soko. Katika siku hizi za kutolewa kwa matangazo, viwango vya kujiinua havirekebishwi, lakini biashara zinaweza kufungwa tu.
Programu ya simu ya JustMarkets
Tambua fursa, fanya biashara na udhibiti akaunti zako za biashara ukitumia programu ya JustMarkets Trade. Furahia urahisi wa kuwekana kutoa pesa, machaguo mengi ya njia za malipo na usaidizi wa ndani ya programu kwa saa 24 siku 7 za juma.
Tumia skana kupakua programu
iOS na Android
Maswali yanayoulizwa mara nyingi
1
Ni nini maana ya hisa?
Hisa inawakilisha umiliki wa sehemu fulani ya kampuni. Unaponunua hisa za kampuni, unanunua sehemu ndogo ya kampuni hiyo, inayojulikana kama hisa. Hisa zinanunuliwa na kuuzwa kwenye masoko ya hisa na ni sehemu muhimu ya uwekezaji mwingi, zikitoa uwezekano wa kukua kupitia kupanda kwa bei za hisa na magawio.
2
Ninawezaje kuanza kufanya biashara ya hisa?
Ili kuanza kufanya biashara ya hisa, kwanza fungua akaunti ya uwakala kwa wakala anayeaminika. Jielimishe kuhusu misingi ya soko la hisa, aina mbalimbali za hisa, na mikakati ya biashara. Anza na akaunti ya majaribio ili ufanye mazoezi bila hatari. Mara utakapohisi umeweza, weka pesa kwenye akaunti yako, anza kidogo kidogo, na ulenge hisa chache ili ujitahidi kufahamu mwenendo wa soko na mabadiliko katika biashara.
3
Soko la hisa linafunguliwa saa ngapi?
Muda wa kufungua masoko ya hisa hutofautiana ulimwenguni pote. Kwa mfano, Soko la Hisa la New York (NYSE) na Nasdaq nchini Marekani hufunguliwa saa 3:30 asubuhi na kufungwa saa 10:00 alasiri Saa za Mashariki (ET). Masoko mengine ulimwenguni kote, kama vile Soko la Hisa la London au Soko la Hisa la Tokyo, yana saa tofauti za kufanya kazi.
4
Ni biashara gani bora kwa wafanyabiashara wanaoanza?
Kwa wafanyabiashara wanaoanza, uwekezaji wa muda mrefu katika hisa mara nyingi hupendekezwa badala ya kununua na kuuza hisa ndani ya muda mfupi. Mbinu hii inahusisha kutafiti na kununua hisa za kampuni imara zilizo na historia ya ukuaji thabiti na kubaki nazo ili ufaidike kutokana na faida za muda mrefu, gawio, na mchanganyiko wa mtaji, faida na gawio.
5
Je, kiwango cha sitisha na kutoka kwa hisa ni kipi?
Kiwango cha kusitisha na kutoka katika biashara ya hisa ni hatua maalum ambapo wakala atafunga papohapo nafasi iliyo wazi kwa bei ya sasa ya soko ili kuzuia hasara zaidi, hasa katika akaunti ya dhamana. Kiwango hiki kwa kawaida huwekwa kama asilimia na hutoa tahadhari wakati dhamana ya mfanyabiashara inaposhuka chini ya kiwango chake, ikidokeza kwamba mtaji wake uliopo hautoshi kugharimia nafasi zilizo wazi.