Nunua na Kuuza Fedha za Kigeni
ukiwa na Tofauti Ndogo & Isiyobadilika Badilika Kati ya Bei ya Kununua na Kuuza

Ingia katika eneo la kimataifa la Fedha za Kigeni na fanya biashara ya jozi bora za sarafu kwa tofauti zenye ushindani kati ya bei ya kununua na kuuza.

Forex hero image

Kwa nini ufanye biashara ya fedha za kigeni na JustMarkets?

benefits-1

Nyenzo nyingi za kupima mabadiliko ya Fedha za Kigeni

Sarafu zaidi ya 60 zinazouzwa zaidi duniani zinapatikana kwa ajili ya kufanyia biashara saa 24 siku 7 za juma.

benefits-2

Biashara ya ubadilishaji bila riba

Kila mfanyabiashara katika JustMarkets anaweza kufanya biashara kwa mfumo wa ubadilishaji bila riba na hakuna matakwa yoyote ya ziada, akiruhusiwa kufanya biashara bila malipo ya ziada.

benefits-3

Tofauti Ndogo & Isiyobadilika Badilika kati ya bei ya kununua na kuuza

Fanya biashara ya fedha za kigeni ya jozi ya sarafu kuu, jozi ya sarafu za kiwango cha chini, au jozi ya sarafu zisizouzwa au kununuliwa kwa ukawaida ukiwa na tofauti ndogo mno kati ya bei ya kununua na kuuza ikianzia kiwango cha chini cha pips 0.0, kuhakikisha utulivu hata wakati ambapo soko linabadilikabadilika mno.

benefits-4

Kutoa fedha papo hapo

Pata pesa zako haraka unapotaka kuzitoa. Chagua kutoka kwenye njia mbalimbali za malipo na upate idhini ya haraka kwa maombi yako.

benefits-5

Ulinzi dhidi ya mabadiliko ya bei yenye athari hasi

Fanya biashara bila wasiwasi ukiwa na ulinzi wetu dhidi ya mabadiliko ya bei yenye athari hasi. Inazuia mabadiliko ya bei yenye athari hasi, kwa hivyo biashara zako huanzia na kuishia pale unapotarajia, bila kukosa mabadiliko yoyote madogo ya bei.

benefits-6

Utekelezaji wa oda haraka

Katika JustMarkets, dili zako zinafanywa papo hapo. Ndani ya sekunde tu, tunahakikisha kuwa biashara zako zinatekelezwa, na kukupa kasi unayohitaji ili kufanya biashara kwa ufanisi.

Tofauti kati ya bei ya kununua na kuuza na ubadilishaji katika soko la fedha za kigeni

Tofauti ya bei wastani

 

pips

Kamisheni

 

kwa kila loti/ndani

Dhamana

 

up to 1:3000

Malipo ya usiku mrefu

 

Pointi

Malipo ya usiku mfupi

 

Pointi

Kiwango cha kuzuia*

 

pips

Hali za soko la fedha za kigeni

Soko la fedha za kigeni ni soko kubwa zaidi la kifedha ulimwenguni, lenye mzunguko wa Dola za Marekani trilioni 5.5 katika miamala ya kila siku. Linapatikana saa 24 kwa siku, Jumatatu hadi Ijumaa, linatoa chanzo endelevu cha fursa za biashara.

Saa za biashara ya fedha za kigeni  

Soko letu la fedha za kigeni linafanya kazi kuanzia Jumatatu 06:02 usiku hadi Ijumaa 5:59 usiku.

Vifaa Kufungua Kufunga
Jozi zote za Fedha za Kigeni Jumatatu 00:02 Ijumaa 23:59

Muda wote upo katika wakati wa seva (GMT+ 2).

Tofauti kati ya bei ya kununua na kuuza

Tofauti kati ya bei ya kununua na kuuza katika soko la fedha za kigeni mara nyingi hubadilikabadilika. Tofauti kati ya bei za kununua na kuuza zilizotajwa hapo juu ni wastani uliopatikana kutoka katika biashara za siku za awali. Angalia tovuti yetu ili kuona tofauti kati ya bei ya kununua na kuuza kwa sasa.

Tofauti kati ya bei za kununua na kuuza zinaweza kuongezeka wakati wa ukwasi mdogo au mabadiliko makubwa katika soko. Hii inajumuisha nyakati kama vile wakati wa mgeuko wa soko, habari mpya kuhusu soko, na matoleo mapya na inaweza kuendelea hadi hali ya kawaida katika soko itakapoanza tena.

Tofauti zetu bora kati ya bei ya kununua na kuuza ni hakika kwenye akaunti yetu ya Raw Spread, ambapo tofauti kati ya bei ya kununua na kuuza huanzia pips 0.0.

Biashara ya Kubadilisha Bila Riba

Riba ya ubadilishaji ni ada inayotozwa kwenye nafasi za biashara za fedha za kigeni ambazo zinabaki wazi usiku kucha. Riba ya ubadilishaji hutofautiana katika jozi tofauti za sarafu. Riba za ubadilishaji hutozwa saa 4:00 usiku GMT+2 kila siku, bila kujumuisha wikendi, hadi nafasi itakapokuwa imefungwa. Ni muhimu kutambua kwamba kwa biashara yenye jozi za fedha za kigeni, riba za ubadilishaji kwa siku ya Jumatano huongezeka mara tatu ili kugharimia gharama za riba za wikendi.

Hutatozwa kwa jozi za sarafu zilizowekewa alama ya “Waliokubaliwa Ubadilishaji bila riba wanaruhusiwa” katika jedwali hapo juu ikiwa una hali ya ubadilishaji bila riba.

Akaunti zote za wateja kutoka nchi yoyote hupewa moja kwa moja hali ya ubadilishaji bila riba.

Kiwango cha kusitisha

Kiwango cha amri ya kusimamisha biashara ndio umbali wa chini zaidi unaokubalika kati ya bei unayotaka kufungua nafasi nayo na bei ya sasa ya soko wakati unapoweka oda inayosubiri (kama vile Zuia Hasara, Chukua Faida, Kuuza kwa amri ya kusubiri bei ipande/ Kuuza kwa amri ya kusubiri bei ishuke, au Kipimo cha kunua kwa bei ya chini/ Kipimo cha kuuza kwa bei ya juu). Kiwango hiki husaidia kupunguza hatari ya mabadiliko ya ghafla ya bei (mtelezo wa bei) wakati wa kipindi cha mabadiliko makubwa ya soko, na huhakikisha utekelezaji wa uhakika zaidi wa oda zinazosubiri.

Zingatia kwamba kiasi katika kiwango cha kusitisha kilichoonyeshwa kwenye jedwali hapo juu kinaweza kubadilika na huenda kisiweze kutumiwa na wafanyabiashara wanaotumia mikakati mahususi ya kuchakata oda nyingi haraka au kutumia Washauri Wataalamu.

Matakwa ya kiasi cha dhamana kisichobadilika

Matakwa ya kiasi cha dhamana kwa jozi za sarafu zisizouzwa au kununuliwa kwa ukawaida hayabadiliki. Ukadiriaji wa kiasi cha dhamana kwa sarafu hizi huamuliwa kulingana na matakwa yake maalumu ya kiasi cha dhamana, na hubaki bila kuathiriwa na mipangilio ya kiwango cha kujiinua ya akaunti yako.

Matakwa ya kiasi cha dhamana kinachobadilika

Matakwa ya kiasi cha dhamana kwa ajili ya akaunti yako yanategemea kiasi cha kijiinua unachochagua. Kurekebisha kiasi chako cha kujiinua kutasababisha mabadiliko yanayolingana kwenye matakwa yako ya kiasi cha dhamana. Vivyo hivyo, kama vile tofauti kati ya bei ya kununua na kuuza inavyoweza kubadilika kulingana na hali ya soko, faida ya kujiinua unayoweza kupata pia inaweza kubadilika. Sababu kadhaa, zilizofafanuliwa hapa chini, zinaweza kusababisha tofauti hizi.

Kiwango cha kujiinua

Mabadiliko ya ukomo wa kujiinua kulingana na mtaji wa akaunti yako:

Mtaji wa akaunti (USD) Maximum leverage
0 – 999 1:3000
1,000 – 4,999 1:2000
5,000 – 39,999 1:1000
40,000 au zaidi 1:500

* Zana za biashara zinaweza kuwa na ukomo tofauti wa kujiinua kulingana na vipimo vyake.

Habari za kiuchumi

Kuanzia dakika 15 kabla ya kuchapishwa kwa habari za kiuchumi zenye athari kubwa hadi dakika 5 baada ya hapo, matakwa ya kiasi cha dhamana kwa ajili ya nafasi mpya zilizofunguliwa kwenye jozi za sarafu za biashara zilizoathiriwa huhesabiwa kwa ukomo wa kujiinua uliopunguzwa.

Unaweza kujua ni wakati gani habari kuu za kiuchumi zinatarajiwa kutolewa kwenye kalenda yetu ya Mambo ya Kiuchumi.

Mgeuko wa soko, wikendi na sikukuu

Sheria ya kiasi cha dhamana kilichoongezwa inatumika pia kwa baadhi ya jozi za sarafu za biashara wakati wa mgeuko wa soko, wikendi, na sikukuu za umma. Jozi hizi za sarafu katika kipindi hiki hutegemea kiasi cha chini cha kujiinua.

Soma zaidi kuhusu matakwa ya kiasi kikubwa cha dhamana hapa.

Programu ya simu ya JustMarkets

Tambua fursa, fanya biashara na udhibiti akaunti zako za biashara ukitumia programu ya JustMarkets Trade. Furahia urahisi wa kuweka na kutoa pesa, machaguo mengi ya njia za malipo na usaidizi wa ndani ya programu kwa saa 24 siku 7 za juma.

Tumia skana kupakua programu

iOS na Android

Phone in a hand

Maswali yaulizwayo mara nyingi

1
Ubadilishaji wa fedha za kigeni ni nini?

Ubadilishaji wa Fedha za Kigeni, au soko la fedha za kigeni, ni soko la kimataifa kwa ajili ya kununua na kuuza sarafu. Linahusisha ununuzi wa sarafu moja wakati wa kuuza sarafu nyingine. Soko hili ni mojawapo ya masoko makubwa na yenye ukwasi zaidi ya kifedha ulimwenguni, ambapo washiriki wanaweza kuwa wafanyabiashara binafsi hadi taasisi kubwa.

2
Ni sarafu gani maarufu zaidi za fedha za kigeni?

Sarafu maarufu zaidi za fedha za kigeni ni sarafu kuu, ambazo ni pamoja na Dola ya Marekani (USD), Euro (EUR), Yen ya Japani (JPY), Pauni ya Uingereza (GBP), Dola ya Australia (AUD), Dola ya Kanada (CAD), Faranga ya Uswisi (CHF), na Dola ya New Zealand (NZD).

3
Jozi za Sarafu Kuu, Jozi za Sarafu za Kiwango cha Chini, na Jozi za Sarafu Zisizouzwa au Kununuliwa kwa Ukawaida Ni Nini?

Katika soko la fedha za kigeni, ‘Jozi za Sarafu Kuu’ zinarejelea jozi za sarafu zinazouzwa sana zinazohusisha Dola ya Marekani, kama vile EUR/USD au USD/JPY. ‘Jozi za Sarafu za Kiwango cha Chini’ au ‘Mikingamo’ ni jozi ambazo hazijumuishi USD, kama vile EUR/GBP. ‘Jozi za Sarafu Zisizouzwa au Kununuliwa kwa Ukawaida’ ni jozi zinazohusisha sarafu moja kubwa na sarafu kutoka kwa uchumi mdogo au unaoibuka, kama vile USD/SGD.

4
Je, ninaweza kufanya biashara ya fedha za kigeni kila siku?

Ndiyo, unaweza kufanya biashara ya fedha za kigeni kila siku. Soko la fedha za kigeni hufanya kazi saa 24 kwa siku, siku tano kwa wiki, likiwaruhusu wafanyabiashara kutenda kupatana na mabadiliko ya sarafu kimataifa wakati wowote ndani ya wiki ya biashara.

5
Ninawezaje kuanza kufanya biashara katika soko la fedha za kigeni?

Ili kuanza kufanya biashara ya fedha za kigeni, jielimishe kuhusu soko la fedha za kigeni na kanuni za biashara. Fungua akaunti ya biashara na wakala maarufu wa fedha za kigeni, fanya mazoezi kwenye akaunti ya majaribio, na kisha uanze kufanya biashara na pesa halisi mara tu unapojiamini. Ni muhimu kuanza na uwekezaji mdogo na kutumia mikakati ya usimamizi wa hatari.

6
Je, kiwango cha kujiinua ni nini katika Soko la Fedha za Kigeni?

Kiwango cha kujiinua katika soko la fedha za kigeni ni zana ambayo inaruhusu wafanyabiashara kushikilia nafasi kubwa wakiwa na kiasi kidogo cha fedha halisi za biashara. Katika biashara ya fedha za kigeni, kiasi cha kujiinua huonyeshwa katika uwiano, kama vile 50:1, 100:1, au 500:1. Inamaanisha kwamba kwa kila dola moja ambayo ni mali yako, unaweza kufanya biashara yenye thamani ya dola 50, dola 100, au ya dola 500.

7
Jinsi ya kuhesabu pips:

Pip, au “asilimia katika pointi,” ni kipimo cha mabadiliko katika kiwango cha ubadilishaji wa jozi moja ya sarafu. Ili kuhesabu pips, unahitaji kuchukua tofauti kati ya bei ya kufungua na kufunga ya biashara yako na kuizidisha kwa kiwango cha ubadilishaji. Kwa jozi nyingi, pip ni nafasi ya nne ya desimali (0.0001).

8
Ukubwa wa fungu la 0.01 unamaanisha nini?

Ukubwa wa fungu la 0.01 katika biashara ya fedha za kigeni, ambao mara nyingi hujulikana kama ‘fungu dogo,’ unawakilisha vipande 1,000 vya sarafu ya msingi. Kwa mfano, katika jozi ya EUR/USD, ukubwa wa fungu la 0.01 utamaanisha euro 1,000.

9
Ada ya ubadilishaji wa Fedha za Kigeni ni kiasi gani?

Ada za ubadilishaji wa Fedha za Kigeni hutegemea wakala na zinaweza kujumuisha tofauti kati ya bei ya kununua na kuuza, tozo kwa kila biashara, au mchanganyiko wa vyote viwili. Baadhi ya mawakala wanaweza pia kutoza ada kwa akaunti kutofanya kazi, kutoa pesa, au nafasi zilizoachwa wazi usiku kucha (ada za riba ya ubadilishaji/mgeuko wa soko). Ni muhimu kuangalia na kulinganisha miundo ya ada kabla ya kuchagua wakala.