Nunua na Kuuza Bidhaa
ukiwa na hali bora zaidi
Panua biashara yako ya uwekezaji kwa kutumia bidhaa zinazoongoza kama vile dhahabu, fedha na mafuta ukiwa na JustMarkets.
Kwa nini ununue na kuuza bidhaa ukiwa na JustMarkets?
Fanya biashara ya bidhaa kwa ujasiri, ukitumia mkakati wowote wa biashara unaoupenda.
Nyenzo mbalimbali za kupima mabadiliko ya thamani za bidhaa
Panua mkakati wako wa uwekezaji kwa kutumia aina mbalimbali za bidhaa tofauti tofauti maarufu kama vile dhahabu, fedha, na rasilimali nyingi za nishati.
Biashara inayoweza kubadilika kulingana na hali
Ingia kwenye soko la bidhaa mbalimbali kwa urahisi, ukinunua na kuuza dhahabu (XAUUSD), fedha (XAGUSD), na Mafuta wiki nzima kwa ajili ya utendaji bora wa biashara.
Usalama wa uwekezaji
Wekeza katika bidhaa zenye Ulinzi wa Salio Chini ya Sifuri. Wakati salio linapofika chini ya sifuri kwa sababu ya mabadiliko makubwa ya ghafla kwenye soko, salio litawekwa sifuri ili kuwalinda wateja dhidi ya hasara zisizotarajiwa.
Ulinzi dhidi ya mabadiliko ya bei yenye athari hasi
Fanya biashara bila wasiwasi ukiwa na ulinzi wetu dhidi ya mabadiliko ya bei yenye athari hasi. Inazuia mabadiliko ya bei yenye athari hasi, kwa hivyo biashara zako huanzia na kuishia pale unapotarajia, bila kukosa mabadiliko yoyote madogo ya bei.
Tofauti Ndogo & Isiyobadilika Badilika kati ya bei ya kununua na kuuza
Fanya biashara ya dhahabu, fedha, au mafuta yenye tofauti ndogo mno kati ya bei ya kununua na kuuza ikianzia pips 0.2, kuhakikisha utulivu hata wakati ambapo soko linabadilikabadilika mno.
Utekelezaji wa oda haraka
Katika JustMarkets, dili zako zinafanywa papo hapo. Ndani ya sekunde tu, tunahakikisha kuwa biashara zako zinatekelezwa, na kukupa kasi unayohitaji ili kufanya biashara kwa ufanisi.
Tofauti kati ya bei za kununua na kuuza na riba za ubadilishaji kwenye soko la bidhaa
Tofauti ya bei wastani
pips
Kamisheni
kwa kila loti/ndani
Dhamana
up to 1:3000
Malipo ya usiku mrefu
Pointi
Malipo ya usiku mfupi
Pointi
Kiwango cha kuzuia*
pips
Hali za soko la bidhaa
Soko la bidhaa ni soko la kimataifa la kununua na kuuza bidhaa mbalimbali kama vile metali zenye thamani na nishati. Biashara inaruhusu kufanya makisio ya bei zinazobadilikabadilika mno za bidhaa kama vile dhahabu na mafuta bila kulazimika kununua mali hiyo, na bila kujali ikiwa bei ya bidhaa inapanda au kushuka.
Saa za kufanya biashara
Soko la bidhaa linafanya kazi kuanzia Jumatatu 07:02 usiku hadi Ijumaa 5:59 usiku, huku jozi fulani zikiwa na ratiba za kipekee. Rejelea yafuatayo kwa ajili ya nyakati maalum za ufunguzi:
| Zana | Kufungua | Kufunga |
| XAGEUR, XAUAUD, XAUEUR, XPDUSD, XPTUSD, XAGUSD, XAUUSD | Jumatatu 01:02 Mapumziko ya kila siku 23:58 – 01:01 |
Ijumaa 23:58 |
| WTI, XNGUSD | Jumatatu 01:02 Mapumziko ya kila siku 23:59 – 01:02 |
Ijumaa 23:59 |
| BRENT | Jumatatu 03:02 Mapumziko ya kila siku 23:59 – 03:02 |
Ijumaa 23:59 |
Muda wote uko katika wakati wa seva (GMT+2).
Tofauti kati ya bei za kununua na kuuza
Tofauti kati ya bei ya kununua na kuuza katika soko la bidhaa mara nyingi hubadilikabadilika. Tofauti kati ya bei za kununua na kuuza zilizotajwa hapo juu ni wastani uliopatikana kutoka katika biashara za siku za awali. Angalia tovuti yetu ili kuona tofauti kati ya bei ya kununua na kuuza kwa sasa.
Tofauti kati ya bei za kununua na kuuza zinaweza kuongezeka wakati wa ukwasi mdogo au mabadiliko makubwa katika soko. Hii inajumuisha nyakati kama vile wakati wa mgeuko wa soko, habari mpya kuhusu soko, na matoleo mapya na inaweza kuendelea hadi hali ya kawaida katika soko itakapoanza tena.
Tofauti zetu bora kati ya bei ya kununua na kuuza ni hakika kwenye akaunti yetu ya Raw Spread, ambapo tofauti kati ya bei ya kununua na kuuza huanzia pips 0.2.
Biashara ya Kubadilisha Bila Riba
Riba ya ubadilishaji ni ada inayotozwa kwenye nafasi za biashara za fedha za kigeni ambazo zinabaki wazi usiku kucha. Riba ya ubadilishaji hutofautiana katika jozi tofauti za sarafu. Riba za ubadilishaji hutozwa saa 4:00 usiku GMT+2 kila siku, bila kujumuisha wikendi, hadi nafasi itakapokuwa imefungwa. Ni muhimu kutambua kwamba kwa biashara yenye jozi za fedha za kigeni, riba za ubadilishaji kwa siku ya Jumatano huongezeka mara tatu ili kugharimia gharama za riba za wikendi.
Hutatozwa kwa bidhaa zilizowekewa alama ya “Waliokubaliwa Ubadilishaji bila riba wanaruhusiwa” katika jedwali hapo juu ikiwa una hali ya ubadilishaji bila riba.
Akaunti zote za wateja kutoka nchi yoyote hupewa moja kwa moja hali ya ubadilishaji bila riba.
*Biashara ya ubadilishaji bila riba haipatikani kwa bidhaa zifuatavyo: XNGUSD, WTI, BRENT.
Kiwango cha kusitisha
Kiwango cha amri ya kusimamisha biashara ndio umbali wa chini zaidi unaokubalika kati ya bei unayotaka kufungua nafasi nayo na bei ya sasa ya soko wakati unapoweka oda inayosubiri (kama vile Zuia Hasara, Chukua Faida, Kuuza kwa amri ya kusubiri bei ipande/ Kuuza kwa amri ya kusubiri bei ishuke, au Kipimo cha kunua kwa bei ya chini/ Kipimo cha kuuza kwa bei ya juu). Kiwango hiki husaidia kupunguza hatari ya mabadiliko ya ghafla ya bei (mtelezo wa bei) wakati wa kipindi cha mabadiliko makubwa ya soko, na huhakikisha utekelezaji wa uhakika zaidi wa oda zinazosubiri.
Zingatia kwamba kiasi katika kiwango cha kusitisha kilichoonyeshwa kwenye jedwali hapo juu kinaweza kubadilika na huenda kisiweze kutumiwa na wafanyabiashara wanaotumia mikakati mahususi ya kuchakata oda nyingi haraka au kutumia Washauri Wataalamu.
Matakwa ya kiasi cha dhamana kisichobadilika
Matakwa ya kiasi cha dhamana kwa biashara zetu za bidhaa ni thabiti lakini yanaweza kubadilika kwa kutegemea kiwango chako cha kujiinua. Ukomo wa kujiinua unaopatikana utatofautiana kulingana na mtaji wa akaunti yako.
- Kwa XAUUSD, XAGUSD, XAGEUR, XAUEUR na XAUUD, ukomo wa kujiinua umewekwa kuwa 1:3000.
- Kwa XPDUSD na XPTUSD, ukomo wa kujiinua umewekwa kuwa 1:100.
- Kwa BRENT, WTI na XNGUSD, ukomo wa kujiinua umewekwa kuwa 1:200.
Matakwa ya kiasi cha dhamana sikuzote hayabadiliki, isipokuwa kwa vipindi maalum vyenye matakwa ya juu ya kiasi cha dhamana.
Matakwa ya kiasi cha dhamana kinachobadilika
Matakwa ya kiasi cha dhamana kwa ajili ya akaunti yako yanategemea kiasi cha kijiinua unachochagua. Kurekebisha kiasi chako cha kujiinua kutasababisha mabadiliko yanayolingana kwenye matakwa yako ya kiasi cha dhamana. Vivyo hivyo, kama vile tofauti kati ya bei ya kununua na kuuza inavyoweza kubadilika kulingana na hali ya soko, faida ya kujiinua unayoweza kupata pia inaweza kubadilika. Sababu kadhaa, zilizofafanuliwa hapa chini, zinaweza kusababisha tofauti hizi.
Kiwango cha kujiinua
Mabadiliko ya ukomo wa kujiinua kulingana na mtaji wa akaunti yako:
| Mtaji, USD | Kiwango cha juu cha kujiinua |
| 0 – 999 | 1:3000 |
| 1,000 – 4,999 | 1:2000 |
| 5,000 – 29,999 | 1:1000 |
| 30,000 + | 1:500 |
*Nishati zina ukomo wa kujiinua unaotofautiana kulingana na vipimo vyake.
Habari za kiuchumi
Kuanzia dakika 15 kabla ya kuchapishwa kwa habari za kiuchumi zenye athari kubwa hadi dakika 5 baada ya hapo, matakwa ya kiasi cha dhamana kwa ajili ya nafasi mpya zilizofunguliwa kwenye jozi za sarafu za biashara zilizoathiriwa huhesabiwa kwa ukomo wa kujiinua uliopunguzwa.
Unaweza kujua ni wakati gani habari kuu za kiuchumi zinatarajiwa kutolewa kwenye kalenda yetu ya Mambo ya Kiuchumi.
Mgeuko wa soko, wikendi na sikukuu
Sheria ya kiasi cha dhamana kilichoongezwa inatumika pia kwa baadhi ya jozi za sarafu za biashara wakati wa mgeuko wa soko, wikendi, na sikukuu za umma. Jozi hizi za sarafu katika kipindi hiki hutegemea kiasi cha chini cha kujiinua.
Sheria ya kiasi cha dhamana kilichoongezwa inatumika pia kwa baadhi ya jozi za sarafu za biashara wakati wa mgeuko wa soko, wikendi, na sikukuu za umma. Jozi hizi za sarafu katika kipindi hiki hutegemea kiasi cha chini cha kujiinua.
Soma zaidi kuhusu matakwa ya kiasi kikubwa cha dhamana hapa.
Programu ya simu ya JustMarkets
Tambua fursa, fanya biashara na udhibiti akaunti zako za biashara ukitumia programu ya JustMarkets Trade. Furahia urahisi wa kuwekana kutoa pesa, machaguo mengi ya njia za malipo na usaidizi wa ndani ya programu kwa saa 24 siku siku 7 za juma.
Tumia skana kupakua programu
iOS na Android
Maswali yaulizwayo mara nyingi
1
Bidhaa ni nini?
Bidhaa ni malighafi au mazao ya msingi ya kilimo ambayo yanaweza kununuliwa na kuuzwa. Zinatia ndani vyanzo vya nishati kama vile mafuta na gesi asilia, metali kama vile dhahabu, fedha, na shaba, na mazao ya kilimo kama vile ngano, kahawa, na sukari. Bidhaa ni mali za msingi zinazotumika katika biashara na mara nyingi ni msingi wa bidhaa na huduma tata zaidi.
2
Ni zana gani zinazoweza kufanyiwa biashara katika soko la bidhaa?
Katika soko la bidhaa, unaweza kufanya biashara ya zana mbalimbali, ikiwa ni pamoja na mikataba ya baadaye, haki ya kununua hisa, mfuko wa biashara ya kubadilishana (ETFs), na mikataba ya tofauti ya bei (CFDs). Zana hizi huwaruhusu wafanyabiashara kukisia kupanda na kushuka kwa bei za bidhaa bila kuzimiliki kihalisi.
3
Ni bidhaa gani inayouzwa zaidi ulimwenguni?
Bidhaa inayouzwa zaidi duniani ni mafuta ghafi. Ni chanzo muhimu cha nishati ulimwenguni na yana jukumu muhimu katika uchumi wa dunia. Mabadiliko ya bei yake yanaweza kuathiri kwa kiasi kikubwa masoko ya kimataifa, na hilo huyafanya yawe bidhaa inayotazamwa na inayofanyiwa biashara zaidi.
4
Je, ni bidhaa zipi 3 bora za kuwekeza?
Kwa kawaida bidhaa tatu bora za kuwekeza zinatia ndani mafuta ghafi, dhahabu, na gesi asilia. Bidhaa hizi ni maarufu kwa sababu ya matumizi yake yaliyoenea, ukwasi wa soko, na uwezekano wa bei kubadilikabadilika mno, mambo yanayoweza kutoa fursa za kupata faida.
5
Ninaweza kuanzaje kuwekeza katika bidhaa?
Ili uanze kuwekeza katika bidhaa, kwanza, jielimishe kuhusu masoko ya bidhaa na mambo yanayoathiri bei za bidhaa. Fungua akaunti ya uwakala ambayo inaruhusu kufanya biashara ya bidhaa, kama vile mikataba ya makubaliano ya kununua hapo baadaye au mikataba ya tofauti ya bei (CFDs). Anza na akaunti ya majaribio ili ufanye mazoezi, na mara utakapohisi umeweza, unaweza kuanza kufanya biashara na pesa halisi, mwanzoni ukilenga bidhaa moja au mbili.
6
Ninawezaje kununua dhahabu kama bidhaa?
Ili kununua dhahabu kama bidhaa, unaweza kuwekeza katika mikataba ya makubaliano ya kununua dhahabu hapo baadaye, mfuko wa biashara ya kubadilishana (ETFs) ya dhahabu, au mikataba ya tofauti ya bei (CFDs) za dhahabu kupitia akaunti ya uwakala. Unaweza pia kununua dhahabu halisi iliyo katika mfumo wa mche au sarafu kutoka kwa wauzaji wanaotegemeka. Kila njia ina faida na mambo ya kuzingatia, kama vile uhifadhi wa dhahabu halisi au uelewa wa uwezo wa kujiinua kwa mikataba ya tofauti ya bei (CFD) za dhahabu.
7
Ni hatari gani kuu zinazoikumba biashara ya soko la bidhaa?
Hatari kuu za biashara ya soko la bidhaa ni pamoja na hali ya soko inayobadilikabadilika mno, hatari za kijiografia, mabadiliko katika mienendo ya usambazaji na mahitaji ya soko, kupanda na kushuka kwa thamani ya sarafu, na athari za hali ya hewa kwa bidhaa za kilimo. Wafanyabiashara lazima pia wajue hatari zinazohusiana na biashara ya kujiinua na ya dhamana.
8
Je, sheria zenu kwa oda zinazosubiri, zuia hasara (ZH), na chukua faida (CF) ni zipi?
Katika biashara ya bidhaa, oda zinazosubiri huwekwa ili kununua au kuuza kwa bei iliyoamuliwa mapema. Maagizo ya Zuia Hasara (ZH) husaidia kupunguza hasara zinazoweza kutokea kwa kufunga nafasi katika kiwango fulani cha bei. Maagizo ya Chukua Faida (CF) hufungia faida kwa kufunga biashara otomatiki mara tu bei itakapofikia kiwango kizuri. Kuweka mipangilio ya ZH na CF kwa ufanisi kunahitaji uelewa wa kubadilikabadilika mno kwa soko na uvumilivu wa hatari.